Mahakama ya Kilifi imetoa kibali cha kukamatwa kwa washukiwa wawili ya kati ya watatu ambao ni raia wa Italia wanaokabiliwa na mashtaka ya unyakuzi wa ardhi baada ya kukosa kufika Mahakamani.
Agizo hilo limetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Charlse Obulutsa baada ya mshtakiwa mmoja kufika mahakamani na kueleza kwaba kesi hiyo haiwezi kuendelea endapo washtakiwa wa kesi hiyo hawako kamili.
Mshtakiwa Armando Tanzini aliagizwa kurudi Mahakamani mnamo tarehe 10 mwezi Disemba mwaka huu ambapo kesi hiyo itasikizwa endapo washtakiwa wenzake ambao ni Pijey Investiment na Pierluigi Caffini watakuwa wameshikwa na kufikishwa mahakamani.
Awali Mahakama ilielezwa kwamba mnamo mwaka wa 1994, washtakiwa hao walifanya uhamisho wa shamba nambari ya usajili Chembe /Kibabamshe /408 yenye thamani ya shilingi milioni 165 miliki ya marehemu Kitsao Mashobo Nyaki kwa kughushi hatimiliki ya ardhi hiyo.
Taarifa ya Tecler Yeri
