ODM yataka ripoti ya NADCO kutekelezwa kikamilifu

ODM yataka ripoti ya NADCO kutekelezwa kikamilifu

Viongozi wa Chama cha ODM wametaka ajenda 10 zilizotiwa saini kati ya Rais William Ruto na Hayati Raila Odinga kutekelezwa kikamilifu kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. 

Viongozi hao wakiongozwa na Kinara wao mpya Dkt Oburu Oginga walisema kutekelezwa kikamilifu kwa ajenda hizo 10 kutaonyesha ukamilifu wa mkataba wa broad-based Government kwa wananchi.

Wakizungumza wakati wa halfa ya kuwapokea wabunge wateule wa Chama cha ODM katika makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi, viongozi hao walisema ripoti ya NADCO imeangazia masuala muhimu yanayomhusu mwananchi.

Hata hivyo Kinara mpya wa chama hicho Dkt Oburu Oginga aliwarai viongozi na wafausi wa ODM kuungana na kushirikiana ili kuhakikisha umaarufu wa chama cha ODM unazidi kushamiri kote nchini.

“Wanachama wa ODM mnafaa kuwa na furaha na ujasiri na pia tunafaa kufanya bidii zaidi kwa sababu kama hatutafanya bidii zaidi na kufanya chama chetu kuwa na umaarufu zaidi basi tutachukuliwa kama watu wasio na maana yeyote”, alisema Oginga.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi