Business
Muungano wa Tuktuk Kwale wapendekeza kutengewa sehemu maalum ya maegesho
Muungano wa waendeshaji wa tuktuk katika kaunti ya Kwale umetaka serikali ya kaunti hiyo kuwatengea sehemu maalum ya kudumu ya maegesho.
Madereva hao walisema kuwa sekta hiyo imekuwa ikichangia pakubwa kwa ukuaji wa uchumi wa kaunti hiyo na kuchangia kiasi kikubwa cha ushuru unaokusanywa na serikali.
Walisisitiza kuwa tuktuk zimekua zikisaidia kusafirisha watalii kufika maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na iwapo wataimarishiwa mazingira ya kazi kutachangia kuimarisha sekta ya utalii pamoja na kuinua maisha ya vijana wengi wanaotegemea kazi hiyo kujikimu kimaisha.
Muungano huo pia ulisema ikiwa hayo yatatiliwa maanani huenda sekta hiyo ya uchukuzi ikaimarika kimapato kwa asilimia pamoja na uchumi wa kaunti hiyo
Taarifa ya Mwanahabari wetu