News

Mung’aro: Miradi yote ya kaunti kukamilika 2026

Published

on

Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Mung’aro amesema serikali yake iko mbioni kuhakikisha miradi yote ya maendeleo katika kaunti inakamilika kufikia mwezi juni mwaka ujao wa 2026.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa makundi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo wanaoishi na ulemavu na wakongwe mjini Kilifi, gGavana Mung’aro alisema miongoni mwa miradi hiyo ni ufunguzi wa uwanja mpya wa michezo mjini Kilifi, uzinduzi wa makao makuu ya kaunti miongoni mwa miradi mingine.

Gavana Mung’aro pia alidokeza kuwa serikali yake inapanga kuanzisha ujenzi wa hospitali ya Ganze ambao utagharimu zaidi ya shilingi milioni 350.

Kiongozi huyo wa kaunti alisema ujenzi wa makao makuu ya kaunti unaendelea na utakapokamilika utarahisisha upatikanaji wa hudumua kwa wakaazi wa Kilifi vile vile kupunguza gharama ya matumizi ya fedha kwa kaunti.

“Kila mradi ambao tumeanza lazima ukamilike kufikia juni 2026, lazima tufungue makao makuu ya kaunti, lazima tufungue kiwanja chetu kipya cha mpira, lazima tufungue hospitali zetu za Mariakani, Kilifi, Bamba, pia tutaanza kujenga hospitali ya Ganze ya zaidi ya shilingi milioni 350”, alisema Mung’aro.

Wakati huo huo alishauri makundi yaliyopokezwa hundi hizo kuhakikisha wanazitumia kuekeza kwenye miradi ya maendeleo ili kuboresha maisha yao vile vile kunufaisha makundi mengine.

“Haya ndiyo mabadiliko tunayoyakusudia tulipoanzisha mfuko wa wezesha, hata hivyo uendelevu wa mfuko huu unategemea ulipaji wa mikopo kwa wakati, kila malipo yanaporejeshwa yanatuwezesha kufadhili makundi mengine yaliyotuma maombi, leo hii tunapozindua rasmi mpango huu wa uzima cash transfer ambao unalenga jamii zetu zisizojiweza hasa wazee katika wadi zote 35, tuko na watu 1,205 kila mmoja atapata shilingi 18,000 ambazo ni malimbikizi ya miezi tisa iliyopita.

Taarifa ya Joseph Jira.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version