News
Mung’aro achaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ODM kaunti ya Kilifi
Uchaguzi wa viongozi wa mashinani wa Chama cha ODM katika kaunti ya Kilifi ulifanyika Agosti 25, 2025 licha ya awali kuhushudiwa vurugu baada ya kutofautiana kwa wafausi wa chama hicho.
Gavana wa kaunt ya Kilifi Gedion Mung’aro alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kilifi na kuchakuwa nafasi ya Teddy Mwambire, baada ya kumbaduliwa uongozini kama Spika wa bunge la kaunti ya Kilifi.
Naibu Mwenyekiti wa chama hicho kaunti ya Kilifi alichaguliwa Joseph Chilumo, Katibu mkuu akichaguliwa Ken Chonga ambaye ni mbunge wa Kilifi Kusini na Mwekahazina akachaguliwa Paul Katana ambaye ni Mbunge wa Kaloleni katika uchaguzi huo wa viongozi wa mashinani wa chama cha ODM katika kaunti ya Kilifi.
Mengine waliochaguliwa ni pamoja na Tima Abuu, Abdallah Kombe, Caro Kalume, Mae Mwadena, Nickson Muramba, Harrison Kombe Twahir Abdul, Rashid Mohamed miongoni mwa viongozi wengine.
Vurugu hizo zilitokea wakati wasimamizi kwenye lango la ukumbi huo wanaoegemea mrengo wa Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro, walipodai kwamba baadhi ya wanachama sio wanachama halisi.
Wafuasi wa Mwakilishi wadi ya Ganda Oscar Wanje ambaye alikuwa anawania wadhifa wa uenyekiti wa vijana kaunti ya Kilifi alilazimika kujiondoa katika wadhfa huo kwani ni kati ya miongoni mwa wale waliozuiliwa kuingia katika ukumbi wa uchaguzi huo na nafasi hiyo ikachaguliwa Abdallah Kombe.
Wafuasi hao walikosoa utaratibu mzima wa maandalizi ya uchaguzi huo, wakishikilia kwamba watawasilisha malalamishi yao kwa kamati kuu ya uchaguzi ya chama cha ODM kupinga uchaguzi huo.
Wafuasi hao wakiongozwa na Mwakilishi wadi ya Ganze Karisa Ngirani, walilaumu utaratibu wa shughuli hiyo, wakisema umekosa kuzingatia haki ya wanachama.
Taarifa ya Mwahoka Mtsumi