Sports

MTG United Wana Malengo ya Kucheza Ligi Kuu

Published

on

Mkufunzi wa kilabu ya akina Dada ya Moving The Goal Post marufu kama MTG United kaunti hii ya Kilifi Fadhili Hamisi marufu coach Tibo amesema kwamba wanalenga kushiriki ligi ya FKFWPL siku za usoni.

Kwenye mahojiano ya kipekee na Kipenga Cha CoCo FM mwalimu huyo ana imani wa kikosi Bora kutimiza malengo hayo. “Nataka MTG United iwe timu ya kwanza ya akina Dada kaunti ya Kilifi kushiriki ligi ya akina Dada nchini kwani Wana uwezo huo.

“Aidha mwalimu huyo amesema licha ya changamoto chungu nzima wanazokumbana za kifedha Lengo lao si kuona tu timu hiyo inapaa Bali pia kuona badhi ya akina Dada hao wanacheza ligi za ndaani na nje za nchi siku za usoni. “Ni wasichana ambao Wana Vipaji itafurahisha sana wakicheza ligi ya ndaani na nje ya nchi hii siku za badaye.

“Vilevile mwalimu huyo ameongezea licha ya Soka akina Dada hao wanapewa mafunzo mengine ikiwemo jinsi ya kuishi vizuri katika jamii,msongo wa mawazo miongoni mwa mengine.

“MTG United haideal tu na soka tuko na vitengo vingine vya kuisaidia makuzi ya mtoto wa kike kama kujitambua katika jamii wanapoingia wakiwa wachanga kuanzia umri wa miaka 9-25.

” MTG United yenye makao hapa mnarani iko nafasi ya Saba ligi ya Supa baada ya kushiriki mechi 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version