Sports
Modric Rasmi Ametua Kwenye Kilabu Ya AC Milan
Kilabu ya AC Milan imethibitisha kunasa huduma za kiungo mbunifu na mzee wa kazi Luka Modric kutoka Real Madrid kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Raia huyo wa Croatia alipasi vipimo vya kimatibabu hapo jana kabila ya kuzinduliwa rasmi ugani San Siro
Mchezaji mwenye umri wa miaka 39 alijiunga na miamba wa uhispania mwaka 2012 akitokea katika kilabu ya Tottenham HotSpurs ambapo amekuwa na mafanikio makubwa mno ikiwemo kushinda mataji zaidi ya kumi na Los Blancos.
Modric ameshinda zaidi ya mataji 10 akiwa na kilabu hiyo ya Uhispania.