News
Afueni kwa wanaoishi na virusi vya HIV
Wakenya walio kwenye hatari ya kuambukizwa virusi vya HIV huenda wakaanza kupokea shindano mpya ya kudhibiti maambukizi kufikia januari mwakani.
Hii ni baada ya shirika la afya ulimwenguni W.H.O kuidhinisha sindano hiyo mpya ambapo Kenya ni kati ya mataifa 9 yatakayoanza kuitumia kwanza.
W.H.O ilitaja Kenya miongoni mwa mataifa yatakayoanzisha sindano ya Lenacapavir dawa ambayo inahitaji kudungwa mara mbili kwa mwaka ili kutoa kinga ya ugonjwa wa ukimwi.
Wazira wa afya nchini Aden Duale alisema Kenya tayari imeweka mikakati kuhakikisha kufikia mwakani wakenya ambao wako katika hatari ya maambukizi wamezuiwa.
Nchi nyingine 8 zitakazoanza kutumia Lenacapavir ni Uganda, Lesotho, Nigeria, Musumbiji, afrika kusini, Eswatini, Zambia na Zimbabwe.
Akitangaza hatua hiyo mjini Kigali nchini Rwanda mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliyataka mataifa hayo kutekeleza kinga hiyo haraka iwezekanavyo.
Taarifa ya Joseph Jira