National News
Miili Iliyofukuliwa Shakahola Imeharibika Kutotambulika
Katibu katika Wizara ya usalama wa ndani Dkt Raymond Omollo amesema baadhi ya miili waliofukuliwa katika makaburi ya halaiki kwenye msitu wa Shakahola kaunti ya Kilifi imeharibika kiasi cha kutambulika.
Omollo amesema japo juhudi zaidi zinaendelea kubaini familia za watu waliopoteza maisha yao kufuatia mahubiri yenye itakadi za kidini, imekuwa vigumu kwa maafisa wa usalama wanaoendesha zoezi hilo.
Katika kikao na Wanahabari, Omollo amewarai wakenya waliopoteza wapendwa wao kutumia fursa hiyo kuhakikisha miili hiyo iliyopo katika makafani ya hospitali kuu ya Malindi inachukuliwa na kuzikwa.
Wakati uo huo, ameahidi wakenya kwamba serikali kupitia idara ya usalama nchini imewekeza mikakati mwafaka ya kuhakikisha taifa linashuhudia uwiano, amani, na usalama wa kutosha katika maeneo mbalimbali.