News

Migos, awataka walimu wakuu wa shule za upili kuwapa wanafunzi vyeti vya masomo

Published

on

Waziri wa Elimu nchini Julius Migos Ogamba amewataka walimu wakuu wa shule za upili kuwapa wanafunzi vyeti vyao vya masomo.

Ogamba vile vile aliwapongeza baadhi ya walimu waliowapa wanafunzi vyeti vyao vya mitihani ya kitaifa licha ya kuwa madeni ya Karo.

Ogamba alisema hatua za baadhi ya shule kutowakabidhi wanafunzi vyeti vyao vya mitihani ya Kitaifa ni kunyume cha sheria.

Akizungumza jijini Mombasa wakati wa kongamano la wakuu wa shule za upili, Ogamba alisema haipaswi kuwa hivyo kwani ni haki ya kila mwanafunzi kupokea cheti pindi tu anapokamilisha mtihani.

“Nachukua fursa hii kuwashukuru nyote hasa wale ambao mliwapa wanafunzi vyeti vyao licha ya wao kuwa na madeni ya karo, ila wakati niliwaambia kuhusu kupeana vyeti kwa wanafunzi hata kama wanadaiwa mlifanya vyema kwa sababu wakati ambapo unashikilia cheti hicho na hujalipwa pesa unazodai bado haina maana nyote mnateseka sababu wewe hujapata pesa unazodai na mwanafunzi pia hana cheti”. …alisema Ogamba.

Taarifa ya Elizabeth Mwende

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version