News
Mahakama ya Kilifi Imeagiza Kuzuiliwa kwa Mshukiwa wa Wizi
Mahakama ya Kilifi imeagiza kuzuiliwa rumande mwanaume mmoja anayekabiliwa na kesi 8 za uvamizi.
Hakimu mkuu wa Mahakama hiyo Ivy Wasike ameagiza mshukiwa huyo kuzuiliwa hadi tarehe 16 mwezi Mei mwaka huu ambapo uamuzi wa kesi hiyo utatolewa.
Awali kabla ya agizo hilo, Mahakama imeelezwa kwamba mshukiwa anayefahamika kama Victor Otieno, alitekeleza kitendo hicho mnamo tarehe 14 mwezi November mwaka 2024 akiwa amejihami kwa bunduki pamoja na kisu na kumjeruhi Reahma Suley Abdillahi kisha kumuibia simu aina ya Samsug pamoja na runinga yenye thamani ya shilingi laki mbili na elfu ishirini na tisa.
Mahakama hiyo pia imeelezwa kwamba mnamo tarehe 27 November mwaka 2024, mshukiwa akiwa maeneo ya Bofa mjini Kilifi aliweza kuiba simu mbili pamoja na tarakilishi tatu mali iliyomilikiwa na Mzigo Abdallah Juma.
Tarehe 26 Machi mwaka huu katika maeneo ya Kilifi, Victor Otieno alitiwa nguvuni na maafisa wa polisi baada ya kupatikana na pingu na kujifanya yeye ni Afisa wa polisi.
Mshukiwa huyo pia anakabiliwa na kesi zengine 5 tarehe tofauti katika Mahakama ya Kkilifi zinazohushisha wizi wa kimabavu pamoja na umiliki wa bunduki aina ya bastola kinyume cha sharia.
Mahakama hiyo pia imeeleza kwamba mshukiwa anakabiliwa na kesi 16 za uvamizi katika Mahakana ya Malindi.