Sports
Madereva Wa KCB Kukabana Koo Rwanda Mountain Gorilla Rally
Madereva zaidi ya 35 kuzindua uhasama katika makala ya mwaka huu ya Rwanda Mountain Gorilla Rally ikiwa ni raundi ya taji la Bara Afrika Julai 4 hadi Julai 6 mjini Kigali Rwanda.
Dereva wa Kenya Karan Patel amesema kwamba anatarajia upinzani mkubwa kutoka kwa Yasin Nasser raia wa Uganda ambaye amejinyakulia pointi 63 na ndiye anaongoza chati mashindano ya magari Barani Afrika,African Rally Championship.
Madereva wengine ambao wako kwenye kinyanganyiro cha kusaka taji hilo ni pamoja na Nikhil Sachania na Carl Flash Tundo ambao wote wanashika nafasi ya pili na alama 50.
Tineja Jeremiah Wahome ameketi nafasi ya nne na pointi 42 akifuatwa na Samman Vohra naye Karan Patel akiketi nafasi ya sita na pointi 35.
Madereva wengine watakaoshiriki ni Michael Muluka wa Uganda na Queen Kalimpinya wa Rwanda.