News

Maadhimisho ya Jumapili ya Matawi

Published

on

Waumini wa madhehebu mbalimbali ya kikristu wamemiminika makanisani kuadhimisha Jumapili ya matawi, juma moja kabla ya maadhimisho ya sikukuu ya Pasaka.

Waumini wa madhehebu ya Anglikana, Orthodox na Lutheran miongoni mwa madhehebu mengine yanaadhimisha Jumapili ya matawi kukumbuka jinsi Yesu Kristu mwana wa Mungu alivyoingia katika mji Yerusalemu, akiwa amepanda punda ishara ya unyenyekevu na amani.

Kulingana na Imani ya dini ya kikristu maadhimisho haya yanaashiria jinsi watu wa Israeli hasa Wayahudi, walivyompokea Yesu Kristu kwa shangwe, wakipeperusha matawi ya mitende na kumtandikia mavazi njiani, wakisema, “Hosana Hosana! Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana!”
Matawi ya mitende ndiyo asili ya jina la siku hii “Jumapili ya Matawi,” ambapo Jumapili ya matawi huashiria mwanzo wa juma kuu; yani wiki ya mwisho ya maisha ya Yesu Kristu kabla ya kuteswa, kufa na kufufuka ambapo waumini wa dini ya kikristu hukamilisha juma hilo na sikukuu ya Pasaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version