Sports
Lyon Yashushwa Ngazi Ligi One Ya Ufaransa
Kilabu ya Olimpiki Lyon Ya Ufaransa imeshushwa ngazi katika ligi hiyo Ligi 1 hadi ligi ya daraja ya pili marufu kama Ligi 2 na chama cha soka cha uchunguzi Ufaransa kwa ubadirifu wa fedha.
Duru za kuaminika zasema kwamba mabingwa hao mara saba wa ligi one wamekua wakitumia hela nyingi kuwasajili wachezaji bila kupata faida yoyote au akaunti zao kupokea hela zozote kwa misimu 2.
Hata hivyo mmiliki wa kilabu hiyo John Texter amesema kwmaba wana imani uamuzi huo utabatilisha kwani wanakwenda kukataa rufaa dhidi ya uwamuzi huo kwa kilabu hiyo.
Lyon walimaliza nafasi ya sita jedwali la ligi ya Ufaransa na walikua kwenye kombe Europa ila huenda hilo likatatiza mipango yao ya msimu ujao.
Kilabu hiyo haijacheza katika ligi daraja ya pili tangu mwaka 1987 na walikua wamepngia kwamba kambi ya mazoezi Julai 7.