Sports

Ligi Kuu Uingereza EPL Kufungua Milango Yake Hii Leo

Published

on

Huku Ligi Kuu Uingereza ikifungua Milango rasmi hii leo usiku kilabu ya Arsenal watakabiliwa na mtihani wa mapema wa kuonyesha uwezo wao wa kupigania taji dhidi ya Manchester United iliyofanyiwa maboresho siku ya jumapili jioni, huku mabingwa watetezi Liverpool ikizindua uhasama wa  msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza nyumbani dhidi ya Bournemouth saa nne usiku.

Newcastle wanatarajiwa kumkosa mshambuliaji wao nyota Alexander Isak, ambaye anataka kuondoka, katika safari ngumu ya ugenini dhidi ya Aston Villa.

Kama Kipenga Cha Coco FM hebu tuangalie kwa undani jinsi timu zimejipanga kuelekea msimu mpya;

Sajili wapya Benjamin Sseko na Victor Gyokeres;Ni washambulizi wawili ambao wengi watakua wanamulika kwa macho ya ndaani kuona jinsi wataongoza safu zao tofauti za mashambulizi,Wawili hao wanatarajiwa kuanza katika timu zao ugani Old Trafford Jumapili hii.

Kilabu ya Arsenal walimumezea mate mshambulizi Sseko akiwa na RB Leipzig kwa zaidi ya mwaka mmoja kabila badaye kumsajili mshambulizi Victor Gyokeres kwa pauni milioni 64.9 kutoka Sporting Lisbon nyota ambaye pia alikua chaguo la kocha Ruben Amorim wa United kwani waliwahi kufanya kazi pamoja.

Vijana wa Mikel Arteta wakiwa wamemaliza misimu mitatu mfululizo bila kushinda taji la EPL wakisaka mfungaji wa kuwasaidia kufunga zaidi.Na mtu wa kuwapa matumaini hayo ni Gyokeres ambaye katika miaka 2 Sporting alifanikiwa kufunga magoli 97 katika mechi 102.

United msimu jana walikua timu mbovu wakimaliza nafasi ya 15 ligi ya Uingereza kwa mara ya kwanza chini ya Amorim ila sasa wamefanya mabadiliko ikiwemo kusajili nyota Matheus Cunha na Bryan Mbeumo wote ambao walingaa msimu jana na Wolves na Brenford Mtawalia.

Ligi hiyo inpoanzaa leo macho ni kwa Liverpool ambayo licha ya kuwa mabingwa na kuondokewa na badhi ya nyota ikiwemo Alexander Trent Arnold,Luis Diaz na Darwin Nunez wameimarisha kikosi chao kupitia kiungo Florian Wirtz kwa pauni milioni 116,beki Jeremie Frimpong na mshambulizi Hugo Ekitite wakivunja rekodi ya matumizi hadi pauni milioni 260 kwa msimu mmoja.

Wakati vilabu vikuu sita na za jadi  Ligi Kuu ya Uingereza—Liverpool, Manchester City, Manchester United, Arsenal, Chelsea na Tottenham—zinavyoendelea kutumia nguvu zao za kifedha kwenye soko la usajili, Aston Villa na Newcastle zimejikuta zikisukumwa pembeni.

Kwa kuwa na vizuizi vya kanuni za uendelevu wa kifedha, usajili mkubwa pekee wa Villa umekuwa ni mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Evann Guessand, aliyejiunga kutoka Nice.

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe, amekuwa akipokea maswali ya mara kwa mara kuhusu hali ya Alexander Isak, ambaye alisusia maandalizi ya msimu mpya akilazimisha uhamisho anaoutamani kwenda Liverpool.

Juhudi za The Magpies kumpata mbadala wa mshambuliaji huyo wa Kiswidi zimegonga mwamba mara kwa mara, huku wachezaji kama Sesko, Mbuemo, Hugo Ekitike, Liam Delap na Joao Pedro wakiamua kujiunga na timu nyingine.

Hata hivyo, katika misimu ya hivi karibuni, Villa na Newcastle wamekuwa wakifanya vizuri zaidi kuliko baadhi ya klabu sita kubwa na msimu huu pia wamelenga kufuzu tena kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ijumaa;

Liverpool v Bournemouth 22:00pm

Jumamosi;

Aston Villa v Newcastle (5:30pm), Brighton v Fulham, Sunderland v West Ham, Tottenham v Burnley, Wolves v Man City (7:30pm)

Jumapili;

Chelsea v Crystal Palace, Nottingham Forest v Brentford (4:00pm), Man Utd v Arsenal (6:30pm)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version