Sports
Leicester Yamfuta Kazi Ruud Van Nistelrooy
Kilabu ya Leicester City imetangaza kuachana na kocha wake Ruud Van Nistelrooy mchezaji wa zamani wa manchester united.
Kocha huyo aliteuliwa mwezi Disemba kumrithi kocha Steve Cooper kutokana na msururu wa matokeo duni ila akashindwa kuokoa kilabu hiyo kushushwa ngazi msimu huu ligi kuu Uingereza.
The Foxes waliboronga na kusuasua wakimaliza nafasi ya 18 na alama 25 na inaminika huenda ikamteua kocha wa zamani wa Everton na Burnley Sean Dyche.