County
Kilifi Imeweka Mikakati Bora ya Kuhakikisha Hospitali na Zahanati Zinakuwa na Madawa ya Kutosha
Naibu Gavana wa kaunti ya Kilifi Flora Mbetsa Chibule amesema serikali ya kaunti ya Kilifi imeweka mikakati bora ya kuhakikisha hospitali na zahanati zote za umma katika kaunti hiyo zinakuwa na madawa ya kutosha.
Chibule amesema tayari serikali ya kaunti hiyo imepitisha bajeti ya fedha za ziadi ili kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia wananchi mashinani, akiwarai wakaazi na wahudumu wa afya kuhakikisha wanalinda madawa hayo.
Akizungumza wakati wa zoezi la uzinduzi wa ujenzi wa jengo la Huduma Centre katika eneo bunge la Ganze, Chibule amesema sekta ya afya hadi mashinani itaboreshwa zaidi.
“Kuna mpango ambao tunaufanya ambao ni kuchukua madawa yetu kutoka KEMSA, japo ule mpango tulikuwa tunataka iko chini ya asilimia 20 lakini madawa yalifika. Nawahimiza wahudumu wa afya na wananchi kulinda raslimali zetu’, alisema Chibule.
Wakati uo huo amepongeza uzinduzi wa ujenzi wa jengo la huduma Centre katika eneo bunge la Ganze, akisema kwamba huduma zote za umma sasa itakuwa zinapatikana kwa urahisi hadi mashinani pindi ujenzi huo utakapokamilika.