Sports
Kilabu Ya KCB Wamemteua Matano kuwa Kocha Mpya.
Kilabu ya Wanabenki Kcb inayoshiriki ligi kuu taifa humu nchini imetangaza kumteua aliyekua kocha wa Tusker FC,Sofapaka na AFC Leopards Robert Matano marufu The Lion kunoa kilabu hiyo msimu ujao.
Matano aliyepigwa kalamu na Fountain Gate ya Tanzania anatwikwa majukumu baada ya kuondoka kwa kocha Patrick Odhiambo aliyeonyeshwa mlango kutokana na msururu wa matokeo duni.
Mwalimu huyo sasa ana kibarua kikubwa cha kurejesha kilabu hiyo yenye senti katika ubora wake baada ya kumaliza nafasi ya tisa ligi ya taifa FKF PL na alama 43.