Sports
Kenya Mabingwa Afrika, Kombe La Catchball
Kikosi cha Taifa cha Kenya mchezo wa Catchball ndiyo mabingwa wa Afrika kombe hilo lililotamatika mjini Soweto Afrika Kusini mwishoni mwa Juma.
Mashindano hayo ambayo ni ya akina dada yalingoa nanga Juni 14-21 yalikua yanajumuisha mataifa ya Kenya,Uganda,Ghana na Afrika Kusini yakilenga kuimarisha mchezo huo katika ukanda wa Afrika kwa jumla.
Kulingana na Rais wa mchezo huo Papa Douglas Shilubane akiwashukuru timu zote za kigeni kwa kuitikia mwito ametaja kuwa lengo lao ni kufanya mchezo wenyewe ujulikane barani.
“Tunalenga kuhahakisha mchezo huu unaenea kote Barani Afrika na kukuja kwenu ni hatua mwafaka wa kuendeleza mchezo huu tulionza hapa Afrika kusini na kueneza kote Barani.”
Kenya ilishinda mechi zake zote tano ambazo alishiriki na hivyo basi kutawazwa kuwa bingwa wa makala hayo ya kwanza.