News
Kanisa lamtaka Rais Ruto kuipa uhuru tume ya EACC
Viongozi wa makanisa wanamtaka rais William Ruto kutimiza vitisho vyake na kuwachukulia hatua wabunge anaodai wanahusika na visa vya ufisadi nchini.
Baraza la makanisa nchini NCCK likiongozwa na naibu mwenyekiti wake Askofu John Okinda akizungumza wakati wa ibada eneo la Roisambu, alimtaka Rais William Ruto kuwasilisha Ushahidi dhidi ya wabunge wanaokula hongo ili wakamatwe.
Pia alimtaka rais William Ruto kuipa tume ya kukabili ufisadi nchini EACC jukumu huru la kufanya kazi yake.
Wakati huo huo muungano mpya wa Kenya Moja ulirai vyama vya upinzani kushikana mkono nao ili kuibandua mamlakani serikali ya rais William Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Wakiongozwa na seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna, mrengo huo wa viongozi wachanga, uliapa kuendelea kusukuma wimbi jipya la wanasiasa wanaopinga sera za Kenya Kwanza.
Hata hivyo baadhi ya mawaziri nchini walijitokeza na kuwasuta wabunge wanaodai kwamba watawasilisha mswada bungeni wa kumtimua rais William Ruto mamlakani kutokana na kauli yake kwamba wabunge ni wafisadi.
Waziri wa kawi na nishati nchini Opiyo Wandayi aliwataka wabunge kusitisha mchakato huo na kujidhihirisha wazi kwa umma kama wao sio wafisadi.
Taarifa ya Joseph Jira