News
Kalonzo, Gachagua Wapinga Ujenzi wa Kinu cha Nuklia Kilifi
Viongozi wa Upinzani wakiongozwa na kinara wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, wamepaza sauti kupinga ujenzi wa kinu cha Nuklia katika eneo la Uyombo wadi ya Matsangoni Kaunti ya Kilifi.
Wakihutubu mjini Malindi Kaunti ya Kilifi viongozi hao akiwemo kinara wa DCP, aliyekuwa Naibu wa Rais Righathi Gachagua na mwenzake wa DAP, Eugene Wamalwa, waliongeza kwamba tayari wamewaagiza mawakili kuwasilisha kesi mahakamani kupinga mradi huo.
Waliyasema haya baada ya kuhudhuria misa ya Jumalipili katika katika Kanisa la JCC iliyoongozwa na Askofu Kakala mjini humo katika siku ya pili ya ziara yao ya ukanda wa Pwani.
Kalonzo alizidisha makombora yake Kwa serikali ya Rais William Ruto akiitaka iwajibikie maovu yake ya visa vya utekaji nyara na mauaji ya Vijana wa kizazi cha Gen-Z wakati wa Maandamano mwaka uliopita.
Kiongozi huyo alisema kwamba mnamo tarehe 25 mwezi huu wa Juni 2025, upinzani utawaongoza wakenya kuwakumbuka vijana waliouawa wakati wa Maandamano hayo ya Gen-Zs mwaka uliopita, kwa kuwasha mishumaa nje ya majengo ya bunge.
Kiongozi wa DCP, na aliyekuwa Naibu wa Rais Righathi Gachagua alisema serikali ya Kenya Kwanza, inaendelea kupora pesa za wafanyi kazi kutoka hazina ya malipoa ya Uzeeni NSSF, na kuzitumia Kwa miradi ya kibinafsi katika eneo la Bomas.

Picha kwa hisani
Kwa upande wake Kiongozi wa DAP, Eugene Wamalwa alisema kwamba serikali ya Rais Ruto sasa inatumia pesa za ushuru wa nyumba kujenga masoko katika Kaunti mbali mbali kama njia Moja wapo ya mbinu za kuwashawawishi viongozi hasa Magavana,kuunga mkono serikali ya KK, na kuongeza Kwamba ujenzi wa masoko ni jukumu la serikali za ugatuzi.
Viongozi hao waliwahutubia wananchi katika soko la Kwajiwa mjini Malindi, huku msafara huo ukisimama eneo la Matsangoni, Chuo kikuu Cha Pwani mjini Kilifi, na mji wa Mtwapa.
Taarifa ya Eric ponda