National News
Jopo la Uteuzi wa Makamishna wa IEBC Lawahoji Waliotuma Maombi
Jopo la uteuzi wa Makamishna wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC limeanza rasmi awamu ya kwanza ya kuwahoji watu waliotuma maombi ya kujaza nafasi ya uwenyekiti wa Tume ya IEBC.
Wakwanza kufika mbele ya jopo hilo kuhojiwa ni Abdulqadir Lorot ambaye ameweka wazi kwamba iwapo atateuliwa kushikilia nafasi hiyo ya uwenyekiti wa Tume ya IEBC atahakikisha Kenya inashuhudia uchaguzi huru na haki.
Mwengine aliyehojiwa ni aliyekuwa Msajali mkuu wa idara ya Mahakama nchini Anne Amadi ambaye ameliambia jopo hilo kwamba ana tajiriba ya uwanasheria kwa zaidi ya miaka 30 hivyo basi ana uwezo wakishikilia nafasi hiyo.
Kuhusu swala la sakata ya dhahabu, Amadi amejitenga na madai hayo akisema sakata hiyo ilikuwa njama ya kutatiza juhudi zake za kuwatumikia wakenya wakati akihudumu katika idara ya Mahakama.
Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Mwenyekiti wa jopo hilo la uteuzi wa makamishna wa IEBC Dkt Nelson Makanda, ambapo aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya utekelezaji wa Katiba Simon Nyachae pia amehojiwa.