News
Joho, asema wanawake wanapaswa kuwezeshwa kimaisha
Waziri wa madini na uchumi wa raslimali za bahari nchini Hassan Ali Joho amesema wanawake nchini wanapaswa kuwezeshwa ili wajiendeleze kimaisha.
Joho ambaye alikuwa akizungumza katika kaunti ya Tana River, alisema mwanamke anapowezeshwa jamii pia inanufaika.
Joho alishikilia msimamo wake wa kumuunga mkono rais William Ruto katika kuwania wadhifa wa urais mwaka wa 2027.
Kulingana na Joho, Rais Ruto amekuwa akitenga fedha za kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo hasa kanda ya Pwani na tayari kuna baadhi ya miradi ambayo imeanza kutekelezwa.
Wakati huohuo, aliwahimiza wakaazi wa Pwani kuwa na umoja na kushirikiana na uongozi wa rais Ruto ili kunufaika kupitia miradi ya maendeleo.
Kauli ya Joho iliungwa mkono na Seneta wa kaunti ya Tana River Danson Buya Mungatana ambaye pia aliwashinikiza wakaazi wa kaunti hiyo kumpigia kura Rais Ruto mwaka wa 2027.
Taarifa ya Janet Mumbi