Taifa la Cameroon limeidhinisha mabadiliko ya kisheria kuhusu wadhfa wa makamu wa rais na kumpa mamlaka zaidi rais wa taifa hilo kufanya uteuzi upya.
Sheria hiyo mpya, inampa uwezi makamu wa rais kuchukua nafasi ya rais moja kwa moja iwapo rais wa taifa hilo amefariki ama amekubwa na ugonjwa na kushindwa kuendelelea na majukumu yake kama rais kabla ya uchaguzi kuandaliwa.
Bunge la taifa hilo siku ya Jumamosi liliidhinisha mabadiliko hayo ya kisheria na kutoa nafasi ya kuteuliwa kwa makamu wa rais ili kuhakikisha shughuli za kiserikali zinaendeshwa vyema baada ya bunge la kitaifa na seneti kupiga kura na kufanya mabadiliko hayo ya kisheria katika taifa hilo la Cameroon.
Wabunge wa bunge la kitaifa na Seneti nchini Cameroon walipiga kura 200 huku wengine 18 wakipinga na wengine 4 wakikwepa kikao hicho cha bunge, hatua iliyopelekea mswada huo kupitishwa.
Hatua hiyo sasa imefanya Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 93 kumteua mwanawe Franck Emmanuel Biya kuwa makamu wa kwanza wa rais katika taifa hilo.

Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 93 na mwanawe Franck Emmanuel aliyemteua kuwa makamu wa rais wa taifa hilo.
Ni hatua ambayo imeibua mjadala mkali nchini Cameroon na bara Afrika kwa jumla baada ya uteuzi huo kutangazwa rasmi Aprili 4, 2026.
Sheria hiyo pia imepiga marufuku wananchi wa taifa hilo kujadili kuhusu hali ya afya ya rais Biya, kukosoa utendakazi wake pamoja na maamuzi yanayofanywa na Ikulu ya rais.
Emmanuel amehudumu katika wadhfa wa mkuu wa majeshi mbali na kushikilia cheo kikuu katika wizara ya ulinzi nchini humo.
Rais Biya amekuwa mamlakani tangu 1982 na alishinda muhula wa nane kwenye uchaguzi mkuu mwaka uliopita.
Kuidhinishwa kwa mabadiliko haya ya kisheria nchini Cameroon kunatambulika kama tukio la kihistoria tangu mwaka 2008 ambapo taifa hilo lilishuhudia pingamizi za kisheria kutoka kwa wananchi baada ya bunge la kitaifa kuongeza hatamu ya uongozi wa rais na kusababisha maandamano makubwa.
Taarifa ya Hamis Kombe
