Mahakama ya Kilifi imemwachilia kwa dhamana ya shilingi laki mbili mshukiwa wa wizi wa kimabavu baada ya kukanusha mashtaka dhidi yake.
Hakimu wa Mahakama hiyo Ivy Wasike ameagiza mshukiwa Hudson Katana kutoa dhamana hiyo na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho.
Agizo hilo limetolewa baada ya upande wa mashtaka ya umma ukiongozwa na Nancy Njeru kuwasilisha uchunguzi Mahakamani.
Awali kabla ya agizo hilo Mahakama ilieleza kwamba mnamo tarehe 10 ya mwezi Mei mwaka huu katika eneo la Makosheni kaunti ya Kilifi mshukiwa akiwa na wengine ambao hawakufikishwa Mahakamani walitekeleza wizi wa kimabavu kwa kumpiga mlalmishi L,ucky Ruwa Chogo na kumwibia pikipiki yake yenye nambari ya usajili KMFK 876V yenye rangi nyekundu aina ya boxer 100 CC ya dhamana ya shilingi laki moja na elfu hamsini.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 26 mwezi Juni mwaka huu na kusikizwa tarehe 22 mwezi Oktoba mwaka huu katika mahakama hiyo ya Kilifi.
Taarifa ya Teclar Yeri
