Maafisa wa kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya kaunti ya Kilifi wafanya oparesheni ya kiusalama na wamewatia nguvuni watu wawili wanaoshukuwa kuhusika na biashara hiyo haramu.
Wawili hao ni pamoja na Esha Mzungu mwenye umri wa miaka 42 na Jamal Chilumo mwenye umri wa miaka 21, ambao wamekamatwa katika eneo la Kisumu ndogo mjini Kilifi wakiwa na magunia matatu ya Mihadarati aina ya bangi.
Kamanda wa Polisi eneo la Kilifi Kaskazini Stanley Tanui amesema wawili hao wametiwa nguvuni wakati wa oparesheni ya kiusalama na kupatikana mihadarati hiyo iliyothibitishwa kuwa ya kilogram 142 na yenye thamani ya shilingi milioni 4.2.
“Maafisa wetu walipata taarifa kutokana kwa wananchi kwamba kuwa watu wanafanya biashara haramu ya ulanguzi wa dawa za kulevya katika eneo la Kisumu ndogo mjini Kilifi na wakaenda hapo na kuwakamata wakiwa na bangi ya tthamani ya shilingi milioni 4.2”, alisema Tanui.

Magunia ya kilo 142 ya Bangi yenye thamani ya shilingi milioni 4.2 imenashwa mjini Kilifi
Tanui aliwaonya watu wenye kuendeleza biashara hiyo haramu, akisema maafisa wa polisi watakabiliana nao kikamilifu ili kukomesha ulanguzi wa Mihadarati kaunti ya Kilifi.
Aidha aliwapongeza wananchi kwa kushirikiana na maafisa wa polisi, akisisitiza kwamba ushirikiano huo utahakikisha unakomesha biashara hiyo haramu.
“Ningependa kuwapongeza wananchi kwa kutoa taarifa kwa maafisa wa polisi na tunaomba waendelee kushirikiana na polisi ili kuhakikisha tunakomesha ulanguzi wa mihadarati.
