Mahakama ya Kilifi imewanyima dhamana washukiwa wawili wa Mahadarati

Mahakama ya Kilifi imewanyima dhamana washukiwa wawili wa Mahadarati

Mahakama ya Kilifi imewanyima dhamana washukiwa wawili wa ulanguzi wa Mihadarati baada ya kukana mashtaka dhidi yao.

Hakimu wa Mahakama hiyo Ivy Wasike, ameagiza wawili hao, Esha Mzungu Kalama mwenye umri wa miaka 42 na Jamal Chilumo Chiriga mwenye umri wa miaka 21 kuzuiliwa rumande baada ya kupatikana na Mihadarati aina ya bangi ya thamani ya shilingi milioni 4.2.

Mahakama imeagiza mshukiwa Esha Mzungu Kalama kuzuiliwa katika gereza la Shimo la Tewa na Jamal Chilumo Chiriga, akiagzwa kuzuiliwa katika gereza la Kilifi, wakati maafisa wa upelelezi wakiendelea na uchukuzi wao.

Uamuzi huo wa Mahakama, umefuatia ombi lililowasilishwa na Kiongozi wa mashtaka ya umma Nancy Njeru, la kutaka washukiwa hao kunyimwa dhamana ili kupeana muda zaidi kwa maafisa wa upelelezi kukamilisha uchunguzi wao.

Mahakama imeelezwa kwamba mnamo 19 mwezi Mei mwaka huu katika eneo la Kisumu ndogo mjini Kilifi kaunti ya Kilifi, wakati wa oparesheni ya kiusalama maafisa wa polisi walifanikiwa kunasa magunia matatu yenye kilo 142 ya bangi katika eneo la Kisumu ndogo mjini Kilifi kaunti ya Kilifi.

Kesi hiyo itatajwa tena mnamo tarehe 27 mwezi Mei mwaka huu.

Taarifa ya Teclar Yeri