China yaishtuma Marekani kwa kuishambulia Iran

China yaishtuma Marekani kwa kuishambulia Iran

Waziri wa mambo ya nje wa taifa la China Wang Yi ametahadharisha kuhusu hatari ya China kutokuelewana na Marekani, akisema hatua hiyo itapelekea kushughudiwa kwa migogoro na makabiliano ambayo yanaweza kuitumbukiza dunia nzima katika janga. 

Wang Yi alitoa kauli hiyo kabla ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kwamba anapanga kuitembelea China mwishoni mwa mwezi huu.

Rais Trump alisema kwamba ana mipango ya kuzuru China kufanya kikao cha mazungumzo na Rais wa taifa hilo Xi Jinping, akilenga kuangazia masuala ya ushirikiano wa kibiashara, usalama, kupunguza ushuru wa bidhaa mbalimbali pamoja na suala la ushirikiano wa kivita.

Kulingana na taarifa kutoka Beijing, huenda ziara hiyo ya Trump ikakosa kufanyika kwani hadi sasa, haijajibu mualiko wa Washington hatua ambayo bado inatia hofu ya ushirikiano wa Washington na Beijing.

Beijing ilieleza kwamba ziara ya Trump nchini China huenda ikaahirishwa kutokana na shambulio la Marekani dhidi ya Iran, ambayo ni moja ya washirika wa kiuchumi wa China.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi