Mahakama ya Sudan Kusini yatupilia mbali pingamizi ya mawakili wa Riek Machar

Mahakama ya Sudan Kusini yatupilia mbali pingamizi ya mawakili wa Riek Machar

Mahakama maalumu nchini Sudan Kusini inayosikiliza kesi ya uhaini, mauaji na dhulma za kibinadamu dhidi ya aliyekuwa makamu wa kwanza wa rais Riek Machar, imetupilia mbali pingamizi la mawakili wa utetezi waliodai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo.

Mahakama hiyo inayoongozwa na jaji James Alala, ikitupilia mbali madai ya Machar, ilisema Machar hana kinga ya kutoshtakiwa.

Mahakama hiyo iliamu kesi hiyo kurejelewa kuanzia jumatano 1, Oktoba 2025.

Mawakili wa Machar, walikuwa wanapinga kesi hiyo kuskilizwa na mahakama hiyo kwa kile walidai ni kesi ya kisiasa.

Aidha Machar alitaka kesi yake kusikilizwa na mahakama  maalum ya Umoja wa Afrikakwa mujibu wa mkataba wa amani wa 2018  uliomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tuhuma dhidi ya Machar zilitokana na waasi waliofanya mashambulizi mwezi Machi 2025, katika eneo la White Nile na kuwauwa wanajeshi 250 akiwemo jenerali wa jeshi la Sudan.

Kesi hii iliibua wasiwasi kuhusu nchi hiyo kurejea kwenye vita.

Taarifa ya Joseph Jira