Kesi ya ufisadi ya Dkt Swazur kuendelea Jumatano

Kesi ya ufisadi ya Dkt Swazur kuendelea Jumatano

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya ardhi Dkt Mohammed Swazur pamoja na wenzake 13 wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani siku ya Jumatano tarehe 4 mwezi Machi mwaka huu.

Swazur pamoja na wenzake wanatarajiwa kufikishwa katika Mahakama ya kukabiliana na ufisadi ya Milimani jijini Nairobi kuhusu sakata za uporaji wa fedha za umma, shilingi milioni 221.3.

Katika kesi hiyo, fedha hizo zinadaiwa kuwa mali ya Shirika la Reli nchini ambayo ilikuwa imetoa fedha hizo kwa Tume ya kitaifa ya ardhi kulipwa fidia wananchi ambao ardhi zao zilichukuliwa kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR.

Watu hao walidai kwamba fedha hizo zilikosa kusambazwa kwa waathiriwa wa mradi huo kusambazwa kwa akaunti za benki za watu binafsi ambao sio walengwa wa mradi huo ikiwemo kampuni binafsi.

Kesi hiyo ya tangu Swazur akiwa uongozini kama Mwenyekiti wa Tume ya kitaifa ya ardhi imekuwa ikiskizwa Mahamakani.

Taarifa ya Mwahoka Mtsumi