Sports

Harambee Starlets Kuelekea TZ Kwa Mechi Za CECAFA

Published

on

Kikosi cha soka akina dada humu nchini Harambee Starlets kimeondoka mapema leo kuelekea mjini Dar es Salaam Tanzania kwa mashindano ya CECAFA baina ya mataifa  Afrika ya Mashriki.

Vipusa hao chini ya kocha Beldine Odemba ilifanya mazoezi mepesi hapo jana kabila ya kukwea pipa hii leo wachezaji 23 wakisafiri ikiwa ni wachezaji wa kimataifa na wanaocheza ligi ya nyumbani.

Starlets wanafungua kampeini Jumapili dhidi ya Burundi kabila ya kumenyana na Uganda ,Sudan Kusini na badaye kumaliza na wenyeji Tanzania.

Kwa mujibu wa kocha Beldine ni kwamba amekichagua kikosi chenye ubora huku badhi ya majina makubwa yakikosekana akiwemo mshmabulizi wa Simba Queens Jentrix Shikangwa,Teresah Engesha pamoja na Mwanahalima Dogo wote wanakosekana kwenye kambi hiyo ya Starlets.

Mechi zote zinapigwa katika uwanja wa Azam Sports Complex mjini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version