Sports

Gilbert Lewa Silipwi Ubuntu Fc.

Published

on

Mkufunzi wa kilabu ya Ubuntu Fc ambaye pia ni mkufunzi wa shule ya Upili ya Majaoni Gilbert Lewa amefichua kwamba halipwi na kilabu yake na kwamba anafanya tu kazi ya kujitolea.

Akizungumza na Kipenga Cha Coco FM mwalimu huyo anasema licha ufanisi ambao wamekua nayo changamoto ni mengi mno kwenye kilabu hiyo.

“Ubuntu silipwi najitolea tu ila ndiyo kilabu imenipa ufanisi na watu kunijua kwa hivyo siwezi nikasema chochote kibaya kwani Ubuntu ni sehemu yangu”.

Hata Hivyo Lewa amesema kwamba Shule Ya Upili Ya Majaoni inamlipa vizuri ndiyo maana akachukua changamoto hiyo mpya akifichua inathiri matokeo ya vijana wake wa Ubuntu Ligi ya Divisheni ya pili kwani hajaenda mazoezini kwa wiki mbili kunoa kilabu yake.

“Majaoni walinitafuta na tukakubaliana na mpaka sasa wananilipa vizuri na tena kwa muda ufao ,Niko na Muda sasa sijaenda kunoa timu ya Ubuntu nilimwachia mwenzangu naambiwa badhi ya wachezaji wanasusia mazoezi kwa sababu mimi ndiyo niliwaleta wanataka kuniona pale uwanjani.”

Ubuntu Fc inaketi nafasi ya sita na alama 33Ligi ya FKF Divisheni ya pili baada ya kutoka sare ya 1-1 na Malindi United.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version