Sports
Florian Wirtz Sasa Mambo Nywee! Kutua Liverpool
Kilabu ya Liverpool imeafikia makubaliano na Bayern Leverkusen kuhusiana na usajili wa kiungo mbunifu Florian Wirtz uhamisho ambao ni rekodi mpya wa uhamisho Uingereza.
Timu hizo mbili zimekua kwenye mazungumzo na sasa kitita cha pauni milioni 116 imeafikiwa kwa tineja huyo mwenye umri wa miaka 22.
Raia huyo Ujerumani sasa atawasili Liverpool kwa ajili ya vipimo vya kimatibabu wiki ijayo na baadaye kutiwa wino kandarasi mpya
Inaaminika Wirtz atamwaga wino mkataba wa miaka mitano na The Reds na kuwa sajili wa pili kwa kocha Arne Slot baada ya kupata sahihi ya beki Jeremie Frimpong wa taifa la Uholanzi kwa pauni milioni 29.5.