Sports
EU Waidhinisha Kuchukuliwa Kwa MotorGP Na Liberty
Bodi ya Bara Ulaya EU limeidhinisha kuchukuliwa kwa mashindano ya mbio za magari MotorGP na kampuni ya Liberty Media ya Marekani ambao pia ni wamiliki wa Formula One.
Haya yanajiri baada ya Kampuni ya Liberty pamoja na Bodi hiyo kutoa taarifa kamili wakithibitisha kuafikiwa kwa makubaliano hayo ambayo yalipata ungwaji mkono mkubwa mno.
Liberty ilikua imeafikia makubaliana na Dorna Sports mwaka 2024 kununuliwa kwa kampuni hiyo ila Bodi hiyo ya bara Ulaya EU ikafungua uchunguzi kuthibitisha uhalali wa ununuzi huo.
Kampuni hiyo yenye makao yake mjini Colorado itamiliki asilimia 84 ya hisa ya MotorGP ,huku Dorna mabyo makau yake ni Madrid nchini Uhispania ikibaki na asilimia 14 ya umiliki wa kampuni hiyo.
Hata hivyo dili hiyo itamalizwa kupigwa sahihi ya mwisho kabila ya Julai 3.