Wimbo Diamond Platnumz na Ciara “Low” umeingia rasmi kwenye chati kubwa za muziki Marekani, ukishika nafasi ya #37 kwenye Billboard Mainstream R&B/Hip-Hop Airplay na #49 kwenye Billboard R&B/Hip-Hop Airplay.
Wawili hao waliungana katika wimbo “Low”, wimbo wa mapenzi unaochanganya mizizi ya R&B ya Ciara na melodi za Kiswahili pamoja na midundo ya kipekee ya Bongo Flava ya Diamond Platnumz.
Hii ni hatua kubwa sio tu kwa muziki wa Tanzania lakini pia kwa Afrika Mashariki. Kwa mara nyengine tena, Diamond anaonesha uwezo wa wasanii wa Afrika Mashariki kutokea kwenye majukwaa makubwa duniani.
Ushirikiano wake na wasanii wa kimataifa kama Ciara unaendelea kufungua milango mipya kwa muziki wa Tanzania na Afrika Mashariki, ukiongeza thamani ya muziki wetu katika soko la kimataifa.

Baadhi ya nyimbo za Diamond Platnumz na wasanii wa kimataifa
- “Wasted Energy” – Alicia Keys ft. Diamond Platnumz.
- “Waka” – Diamond Platnumz ft. Rick Ross.
- “Nana” – Diamond Platnumz ft. Flavour (Nigeria).
- “Inama” – Diamond Platnumz ft. Fally Ipupa.
- “Kidogo” – Diamond Platnumz ft. P-Square (Nigeria).
- “African Beauty” – Diamond Platnumz ft. Omarion (USA).
- “Marry You ” – Diamond Platnumz ft. Ne-Yo (USA)
