Futeni DEDE Mrudi Studio, Presenter Kai kwa Kilifi One

Futeni DEDE Mrudi Studio, Presenter Kai kwa Kilifi One

Muunda maudhui maarufu kutoka Kenya, Presenter Kai, amewataka wasanii waliojitokeza kwa pamoja kutengeneza wimbo DEDE, Kilifi One, kuufuta kwenye mitandao na kurudi tena studio.

Kai, ambaye ni gumzo sasa kwa maudhui yake ya MY WIFE, amesema utunzi wa wimbo huo haukidhi viwango vya ubora unaostahili na umeacha maswali kuhusu ubunifu wa wasanii hao.

“Mmeshikana vizuri, mmeenda studio tukidhani mnafanya kitu kizuri. Kumbe mnatuletea wimbo mbovu — halafu bado mkapata ujasiri wa kuuachia! Kwa nini hamkushauriana?” alisema Presenter

Video ya Wimbo DEDE uliotungwa na kundi la wasanii wa Kilifi akiwemo PDay na AlKenia Luv Chante ulipakiwa kwenye mtandao wa YouTube siku tatu zilizopita na hadi kufikia wakati tunaachia taarifa hii ulikuwa na 1.9K views.

Katika kuelezea dhamira yao, PDay alipost kwenye akaunti yake ya Facebook akisistiza  kuwa kazi hiyo ya DEDE si tu jaribio la kufufua ari ya tasnia ya muziki, bali pia ni hatua ya kujifunza kujitegemea na kujiongoza.

Alisema wengi hawajui namna ya kuanza kujisaidia, lakini wakiongozwa kwa mfano mzuri, watapata ujasiri wa kufanya vivyo hivyo.

“Tunatoa kazi hii si kwa ajili ya kufufua tasnia pekee, bali pia kama njia ya kujifunza kujitegemea — jambo ambalo wengi wetu hatujui jinsi ya kulifanya. Watu watafanya hivyo hasa baada ya sisi kuongoza kwa mfano.”