News

‘Chungwa’ lawanyaukia kwa baadhi ya viongozi wa ODM Kilifi

Published

on

Mwakilishi wadi ya Malindi mjini Rashid Odhiambo amekiri kuwepo kwa mvurugiko mkubwa ndani ya chama cha ODM katika kaunti ya Kilifi.

Akizungumza katika kipindi cha Coco Asubuhi siku moja baada ya kura za viongozi wa mashinani wa ODM, Odhiambo alikiri kuwa kumekuwa na hali ya viongozi wa awali wa chama hicho kufinyiliwa kinyume na matarajio.

Odhiambo alisema ni wazi kuwa kumekuwa na mikakati ya kusambaratisha viongozi waliosimama na chama hicho kwa muda mrefu

Alieleza kugadhabishwa na tukio ambapo baadhi ya wagombea wa nyadhfa mbalimbali kwenye chama hicho walizuiliwa pamoja na wafuasi wao.

Aliongeza licha ya wao kutumia njia mwafaka za kuelekeza lalama zao kufuatia mivutano inayoshuhudiwa jitihada zao zimeonekana kuambulia patupu.

Odhiambo aidha aliwashauri wananchi sasa kutozingatia misingi ya vyama katika kuwachagua viongozi.

Taarifa ya Hamis Kombe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version