Sports
Chama Cha Raga KRU Yapata Mwenyekiti Mpya
Chama Cha Raga nchini KRU kimemtangaza Harriet Okach kuwa mwenyekiti mpya kwenye shirikisho hilo kumrithi Sasha Mutai aliyejiuzulu wadhifa wake wiki jana.
Uteuzi huo uliothibitishwa siku ya Alhamisi inamaana kwamba Okach anakua mwanamke wa kwanza kuwa mwenyekiti katika Shirikisho hilo la mchezo wa Raga nchini KRU.
Kabla ya kuteuliwa kwake Okach amekua msimazi wa mauzo kwenye shirikisho hilo,na sasa amesema kwamba analenga kuboresha shirikisho hilo na mchezo kwa jumla anachukua hatamu ya uongozi.
“Nataka nichukue fursa hii kuwashukuru nyote kwa kunipa nafasi hii kwanza shirikisho KRU,washikadhau nimeheshimika mno na nimeahidi sitawangusha ,matumaini yangu ni kufanya Mchezo wa Raga na wachezaji wa Raga kuwa katika mandhari mazuri siku za usoni.”
Mutai alijiuzulu wadhifa wake katika Shirikisho hilo kwa kile alichokitaja ni kutopata ungwaji mkono baina ya washikadau wa mchezo huo nchini.