Wakulima waombwa kukumbatia teknolojia katika ufugaji

Wakulima waombwa kukumbatia teknolojia katika ufugaji

Waziri wa Kilimo, Mutahi Kagwe, amesisitiza umuhimu wa wakulima nchini kukumbatia teknolojia ya kisasa katika shughuli zao za ufugaji, akisema kuwa hiyo ndiyo njia bora ya kuinua kiwango cha uzalishaji na kuimarisha nafasi ya Kenya katika masoko ya kimataifa.

Akizungumza jijini Mombasa wakati wa kikao cha baraza la magavana, waziri Kagwe alisema matumizi ya teknolojia ya kisasa ni hitaji muhimu kwa wakulima wanaotaka kufikia viwango vinavyohitajika katika masoko ya kimataifa ya bidhaa za mifugo.

Alisema kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo inalenga kutenga bajeti maalum kwa ajili ya utoaji wa chanjo kwa mifugo, hatua ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa kuboresha afya ya wanyama na kuongeza ubora wa bidhaa zinazotokana na mifugo.

Aidha, waziri Kagwe alitoa wito kwa taasisi za utafiti wa kisayansi nchini kuhakikisha kuwa shughuli zao zinaangazia kwa undani mahitaji halisi ya sekta ya ufugaji, ili kusaidia wakulima kupata suluhisho kwa changamoto mbalimbali ikiwemo chakula kinachofaa kutumika kwa mifugo.

Aidha, Waziri Kagwe alitoa wito kwa taasisi za utafiti wa kisayansi nchini kuhakikisha kuwa shughuli zao zinaangazia kwa undani mahitaji halisi ya sekta ya ufugaji, ili kusaidia wakulima kupata suluhisho kwa changamoto mbalimbali ikiwemo chakula kinachofaa kutumika kwa mifugo.

Taarifa ya mwanahabari wetu