Watu saba wanazuiliwa na maafisa wa polisi katika eneo la Rabai kaunti ya Kilifi baada ya kukamatwa kwa madai ya kufanya uchawi katika kijiji cha Buni, Kibaoni.
Saba hao wanajumuisha msichana mwenye umri wa miaka 25.
Kundi hilo lilipatikana na maafisa wa polisi wakifanya matambiko katika boma la Mzee Mburusi Gibson na vitu vya ajabu vinavyohusishwa na uchawi.
Watu hao walipatikana wamekita kinu kilichofungwa kwa vitambara vyekundu na kisha kuzungushiwa majani ya mgomba katika mlango wa boma hilo.
Saba hao wanajumuisha Tobias Kassim Ngao mwenye umri wa miaka 53, Mrisa Nyae Chaka ambaye ni mganga maarufu kutoka kaunti ya Kwale, Ali Mchonyi Mwantsaka, Ngoka Kumbiro Chilonga, Omari Kombira Kimboga, Happy Menza Pola na Nachiro Chitsava.
Wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani baada ya polisi kukamilisha uchaguzi dhidi yao.
Taarifa ya Mwanahabari wetu
