Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amesema kunahaja ya serikali kuu kuhusisha maoni ya umma katika suala la raslimali za madini kabla ya kuruhusu waekezaji kuanza kuchimba raslimali hizo.
Baya alisema wakaazi wa eneo husika wanafaa kupewa fursa ya kufahamu namna watakavyofaidika na raslimali hizo hasa iwapo zinapatikana katika ardhi zao.
Mbunge huyo ambaye pia ni naibu kiongozi wa wengi katika bunge la kitafa, alisema viongozi hawafai kuwatenga wananchi katika mjadala huo, akisema eneo la pwani linaraslimali nyingi ambazo kufikia sasa hazijamfaidi mpwani.
Matamshi yake yanajiri huku kukiwa na mgogoro wa uchimbaji madini katika eneo la Dzombo kaunti ya Kwale, ambapo uongozi wa kaunti umekuwa ukishinikiza umuhimu wa wakaazi wa eneo hilo kuhusishwa kabla ya zoezi la uchimbaji kuanza.
Taarifa ya Joseph Jira
