Waziri Migos Ogamba aonya walimu wakuu

Waziri Migos Ogamba aonya walimu wakuu

Waziri wa elimu nchini Migos Ogamba ameonya wakuu wa shule wanaolazimisha wazazi kununua sare katika maduka maalum.

Waziri Ogamba alisema hali hiyo inakiuka kaununi zilizowekwa na serikali huku akiwataka wazazi kuripoti walimu hao.

Alikiri kuwepo malalamishi kutoka kwa wazazi kuhusu kuongezeka kwa gharama za vifaa vya shule akisema limechangiwa na jinsi baadhi ya wakuu wa shule wanavyolazimisha wazazi kununua vifaa maalum kutoka sehemu husika.

Wakati huo huo waziri Ogamba alisema asilimia 85 ya wanafunzi tayari wameripoti kujiunga na gredi ya 10 katika shule za umma nchini huku zoezi la kukusanya takwimu za waliojiunga na shule za kibinafsi likiendelea.

Taarifa ya Joseph Jira