Wavuvi wa eneo la Pwani wameitaka serikali kuu na zile za kaunti kuwatafutia masoko ya kimataifa kwa ajili ya bidhaa zao za samaki.
Wavuvi hao walisema licha ya kuwa na rasilimali kubwa ya samaki baharini, wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa masoko hali inayosababisha samaki kuharibika na kupelekea kuuzwa kwa bei ya chini sokoni.
Walieleza kuwa kuanzishwa kwa masoko ya kimataifa kutawasaidia kupata faida zaidi, kuongeza ajira kwa vijana na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo ya pwani.
Walitaka pia serikali kushirikiana na sekta binafsi kuwekeza katika miundombinu ya uhifadhi wa samaki, teknolojia ya usindikaji na usafirishaji ili bidhaa hizo zikidhi viwango vya kimataifa.
Taarifa ya Pauline Mwango