Benki kuu ya Kenya yabuni kitengo cha kukabili ulaghai wa kifedha mtandaoni

Benki kuu ya Kenya yabuni kitengo cha kukabili ulaghai wa kifedha mtandaoni

Utafiti wa udhibiti wa sekta ya fedha humu nchini uliotolewa na benki kuu ya Kenya unaonyesha kuwa uwekaji mifumo ya kifedha mitandaoni inachangia kwa mchipuko wa uhalifu ikiwemo ubadilishaji wa kadi na udukuzi wa taarifa za wateja.

Kulingana na ripoti hiyo wadukuzi waliiba shilingi bilioni 1.6 za wateja hali inaoashiria hali ya hatari kwenye shughuli za ubadilishanaji wa fedha mtandaoni na kwenye simu.

Aidha ripoti hiyo inaonyesha kuwa udukuzi wa taarifa za wateja umechangia hasara ya shilingi milioni 199.1 huku taasisi za kifedha zikilazimika kulipa kati ya shilingi 80 na shilingi milioni 400 kila mwaka.

Ili kukabiliana na hatari hiyo, benki kuu ya Kenya imebuni kitengo cha kukabiliana na ulaghai wa kifedha mtandaoni.

Benki hiyo ilisema kuwa kitengo hicho ni nguzo muhimu ya utekelezaji wa kanuni za matumizi mabaya yatarakilishi pamoja na uhalifu wa mtandao za mwaka 2024.

Taasis za kifedha zilitakiwa kuzingatia kanuni hizo na kutoa taarifa kuhusu visa vya uhalifu mtandaoni kwa benki hiyo.

Taarifa ya Pauline Mwango