Sports
Bruno Akataa Al-Hilal
Ni taarifa nzuri kwa mashabiki wa kilabu ya Manchester United kwani ,Kiungo na nahodha wa kilabu ya Manchester united Bruno Fernandes amekataa ofa ya pauni milioni 200 kutoka kilabu ya Al-Hilal ya saudia.
Mabingwa hao walikua wametoa ofa hiyo na ada ya ununuzi ya pauni milioni 100 kwa kilabu ya United kupata sahihi ya mchezaji huyo ila inaaminika familia imekua sababu kuu ya Mreno huyo kudinda kuondoka england.
Timu hiyo ilikua imempa kiungo huyo makataa ya wiki moja kuamua iwapo atajiunga nao au la. Hata hivyo baada ya kuketi mezani na mawakala wake na kilabu ya Manchester United inaaminika kwamba mchezaji amekubali kusalia barani Ulaya.
Kilabu ya Al-Hilal ilikua tayari kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 mkataba wa miaka mitatu na mshahara mnono kujiunga nao msimu ujao ila uwamuzi huo umepokelewa vyema na usimamizi wa United ambao hawakua tayari kumwachilia nyota huyo.