News

Joho, awahimiza wakenya kujisajili katika “Boma Yangu”

Published

on

Waziri wa Madini na Uchumi wa raslimali za bahari Ali Hassan Joho, aliwahimiza wakenya kujisajili katika mpango wa “Boma Yangu” ili kunufaika na nyumba za bei nafuu zinazojengwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Waziri Joho alipongeza mradi huo wa serikali, akisema unalenga kuwaondoa wakenya kutoka kwenye makaazi duni na kuwapatia makaazi bora yenye hadhi na mazingira salama ya kuishi.

Akizungumza katika kaunti ya Mombasa baada ya swala ya Eid-ul-Adha, Joho aliwahimiza wakaazi wa eneo la Pwani kuchukua hatua za haraka kujisajili ili wasikose fursa hiyo muhimu ya kuboresha maisha yao.

“Kuna huu mradi unaitwa Affordable Housing, huu mradi mmeona umefanywa mahali kwingi sana na sai usajili wa ule mradi ambao utafanyika pale VOK eneo bunge la Nyali, nyumba 1,976 zitajengwa na mambo mengine, nawasihi kwa heshima kubwa sana waingie kwa Boma Yangu wajisajili”, alisema Joho.

Kwa upande wake Kamishna wa kaunti ya Mombasa Mohamed Nur aliwahimiza vijana kujitokeza kwa wingi kutuma maombi ya nafasi za ajira katika mpango wa kazi mtaani kwa vijana.

Taarifa ya Mwanahabari wetu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version