National News

Bodi ya HELB yatoa shilingi bilioni 1.56 kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu

Published

on

Waziri wa Elimu nchini Julius Migos amesema Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini HELB imetoa shilingi bilioni 1.56, kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya TVET kote nchini.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Waziri Migos amesema pesa hizo zilitolewa tangu siku ya Ijumaa wiki iliyopita huku ikiwaangiza wanafunzi waliokuwa wamewasilisha maombi kuangalia kaunti zao za benki.

Taarifa hiyo imesema Wanafunzi 31,263 wa vyuo vya kiufundi vya TVET wamenufaika na ufadhili huo na wanafunzi 33,863 wakiwa wa vyuo vikuu, huku ikisema kwamba hatua hiyo itawawezesha wanafunzi hao kuendelea na masomo yao.

Kulingana na taarifa hiyo, mwaka huu wa fedha wa 2024/2025 bodi ya HELB nchini imetoa jumla ya shilingi bilioni 32.7, pesa ambazo zimewafaidi wanafunzi wa vyuo na kwamba hatua hiyo itawezesha wanafunzi wanaotegemea mikopo kufanikisha elimu ya juu bila kukatizwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version