News

Mahakama kuu Imeagiza Kutoapishwa kwa Makamishna wa IEBC

Published

on

Mahakama kuu imeagiza kutoapishwa na kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali majina ya Makamishna wapya wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Jaji wa Mahakama hiyo Lawrence Mugambi, ameliagiza bunge la kitaifa kuwapiga msasa Makamishna hao pamoja na Mwenyekiti mpya wa IEBC waliyopendekezwa na jopo la uteuzi la IEBC baada ya zoezi la kuwahoji kukamilika.

Jaji Mugambi amesema masuala yaliyoibuliwa katika kesi hiyo yana uzito na pia yanahusisha wananchi hivyo basi Mahakama haiwezi kuyapuuza kwani yanahitaji ufafanuzi wa kisheria na Katiba.

Jaji Mugambi hata hivyo amewasilisha faili ya kesi hiyo kwa Jaji Mkuu nchini Martha Koome ili kuteua jopo la majaji watatu watakaosikiliza na kuamuzi kesi hiyo.

Kesi hiyo iliwasilishwa Mahakamani na Wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu Boniface Mwangi na Kelvin Roy Omondi, wakilishtaki bunge la kitaifa, Mkuu wa utumishi wa umma pamoja na watu wengine wanane.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Trending

Exit mobile version