News
SHILINGI MILIONI 600 ZATENGEWA MRADI WA BANDARI NDOGO ENEO LA VUMA
Serikali ya kitaifa kupitia wizara ya uchumi na raslimali za baharini na maziwa imetenga kima cha shilingi milioni 600 ili kuanzisha mradi wa bandari ndogo katika eneo la Vuma, Takaungu, Mnarani, Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi.
Akizungumza na coco fm, mwenyekiti wa wahudumu wa maboti Kilifi mjini kaunti ya Kilifi, Shallo Issa amebainisha kuwa walituma maombi kwa serikali kuu wakiomba bandari ndogo inayotumika na wawekezaji wa kibinafsi kule Mnarani iwekewe mikakati ya kumilikiwa na mamlaka ya bandari nchini pindi uwekezaji huo utakapokwisha.
Shallo akisema kuwa bandari hiyo inaweza kutumika kwa namna nyingine ili kuimarisha wavuvi wa Mnarani na Kilifi Lakiji pia njia mojawapo ya kuimarisha uchumi wa baharini eneo hili.
Aidha Shallo amesema kuwa bandari hiyo itasaidia sana katika kubuni nafasi za ajira kwa vijana kwenye sekta ya uvuvi.