News
Mahakama ya Kilifi Imeagiza Kuzuiliwa Rumande Mshukiwa wa Unajisi
Mahakama ya Kilifi imeagiza kuzuiliwa rumande kwa mshukiwa wa unajisi wa mtoto umri wa miaka 7 wakati kesi hiyo ikiendelea.
Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo Ivy Wasike ametoa agizo hilo akisema mshukiwa huyo anafaa kurudishwa Mahakamani mnamo tarehe 29 mwezi Mei mwaka huu.
Kabla ya agizo hilo, Mahakama imeelezwa kwamba mnamo tarehe 6 mwezi Februari mwaka huu mshukiwa Julius Mramba alitekeleza kitendo hicho katika maeneo ya Matsangoni kaunti ya Kilifi.
Mahakama pia imeelezwa kwamba mshukiwa alitekeleza unyama huo baada ya kuandamana na mtoto huyo hadi shambani kuchukua Nazi alizokuwa ameagizwa na mama wa mtoto huyo.